WASTARA ATOKEWA NA SAJUKI KITANDANI
SIKU chache baada ya staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma
kumaliza eda na kurejea Bongo akitokea Uarubuni ameanza kuona maruweruwe
ndani ya chumba alichokuwa akilala na mumewe marehemu, Sadick Juma
Kiwoloko ‘Sajuki’, Risasi Mchanganyiko lina habari za uhakika.
Kwa mujibu wa Wastara siku hiyo akiwa amelala chumbani humo, usiku wa manane alihisi uwepo wa Sajuki kitandani kwake.
“Niliongea
naye kwa kweli siwezi kukumbuka haswa ni nini tulichoongea lakini
tulikuwa katika hali ya furaha sana,” alisema Wastara.
Pia, Wastara
alisema kuwa wakiwa katika maongezi yao, aliuchukua mkono wake na
kuuweka juu ya mwili wa Sajuki katika hali ya mapenzi na akapitiwa na
usingizi.
“Asubuhi nilipoamka nilihisi kama nilikuwa na Sajuki pale
kitandani, kuangalia vizuri, mkono wangu ulikuwa juu ya shuka badala ya
mwili wa Sajuki,” aliongeza.
Hata hivyo, Wastara alisema kuwa alihisi
ni ndoto lakini alipochunguza alihisi kama kulikuwa na mtu aliyekuwa
amelala naye pale kitandani.
“Sijui kama ni maruweruwe, ndoto au
Sajuki alikuja kweli kitandani kwangu, kikubwa ninachokiamini ni kwamba
mapenzi kwa marehemu mume wangu ndiyo yamepelekea hali hiyo,” alisema.
No comments:
Post a Comment