Wasanii wa Maigizo wanaounda Kundi la Origino Komedi hii leo wameingia Makubaliano ya usimamizi na Kampuni ya NEXUS Consulting Agency kwa Kushirikiana na Rockstar 4000 kwa lengo la kuwawezesha kuboresha zaidi kazi zao.
Akizungumza Jijini Dar es salaam mara baada ya kusainiwa kwa Mkataba huo, Mkuu wa Kitengo cha Vipaji na Uendeshaji wa Biashara, ROCKSTAR4000, CHRISTINE MOSHA amesema wameingia makubaliano na Kundi hilo ikiwa ni namna moja wapo ya kukuza na kuendeleza vipaji na Sanaa kwa ujumla kutoka ilipo sasa na kuwa ya Kimataifa.
Kwa upande wake Muandaaji wa vipindi vya Origino Komedi, SEKIONI DAVIS, amesema Mkataba huo utawawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi na kufikia malengo yao ya kukidhi haja ya Soko nchini na kwingineko Ulimwenguni.
No comments:
Post a Comment