msimu wa burudani Highlands fm 92.7

msimu wa burudani Highlands fm 92.7

Thursday, June 06, 2013

JOHA KASSIM KUJIKITA KATIKA FILAMU






MWANADADA anayeng’ara katika tasnia ya muziki wa taarabu nchini, Joha Kassim, wa kundi la T-Moto, amesema amegeukia tasnia ya filamu ili kuonyesha kipaji chake kwa mashabiki.
Akizungumzia swala hilo, Joha amesema ameamua kufanya hivyo ili kuonyesha kipaji chake na kwamba yeye ni msanii na anajua nini anachokifanya katika fani hizo ambapo ana uhakika anafanya vitu vinavyopendwa na jamii.
“Mimi kama msanii natakiwa kuonyesha kipaji changu, filamu hii ni ya kwanza kucheza, nimecheza na Muhogo Mchungu, najua wasanii wa filamu wakiiona hii, watanitafuta kutaka nicheze filamu zao, nina uhakika na nilichokifanya ndani yake,” alisema.
Joha, aliwataka wapenzi wa filamu nchini, kumpokea vizuri katika tasnia hiyo pamoja na kumpa sapoti katika kazi zake.
Kundi la T-Moto Taarabu, kwa sasa linatamba na kibao chao cha ‘Domo la Udaku’ ambacho kinafanya vizuri katika tasnia ya muziki huo na pia linajiandaa kukamilisha kazi yao mpya inayojulikana kwa jina la ‘Kuna Mungu sio Miungu’.

No comments:

Post a Comment