msimu wa burudani Highlands fm 92.7

msimu wa burudani Highlands fm 92.7

Sunday, June 23, 2013

MBOTO ASAINI DILI NA LEO MEDIA


Mboto msanii mkali wa comedy kwenye tasnia ya bongomovie amesaini mkataba wa mwaka mmoja kufanya kazi na kampuni ya Leo Media. Leo Media ni kampuni mpya inayohusika pia na kusambasa filamu za bongomovie. Leo Media imeshasambaza filamu kama Waiting Soul,Babylon na nyingine nyingi. Wasanii wengi wamekuwa na kilio cha kutokuwa na wasambazaji wengine watakaoweza kuwapa chaguo lingine la kuwasambazia kazi zao, Leo Media imejipanga kuja kufanya kazi vizuri na wasanii wa filamu Tanzania. Akiongea production manager wa Leo Media bwana Geoffrey Kusila baada ya kusaini mkataba na Mboto alisema kwamba, Leo Media inakusudia kufanya kazi karibu na wasanii wenye zaidi ili kuhakikisha waipeleka bongomovie kwenye hatua nyingine. Filamu ya kwanza kutoka kwa Mboto itakayo sambazwa na Leo Media ni Bana Congo ambapo Mboto ameigiza kama mhamiaji haramu kutoka Congo na anaishi Dar.

IMG_3582
Baada ya kusaini Mkataba wa makubaliano ya kufanya kazi
IMG_3585 Production Manager wa Leo Media akisaini kwa niaba ya Leo Media IMG_3589
Mboto akitisaini mkataba wa makubaliano
IMG_3591

IMG_3594

No comments:

Post a Comment