NORA AMPIGA MHUDUMU WA HOTELI
STAA wa filamu za Kibongo, Nuru Nassoro ‘Nora’ anadaiwa kumzaba makofi
mhudumu wa Hoteli ya Lunch Time, Mabibo, Dar aliyetajwa kwa jina la
Joyce Mashika.
Katika tukio hilo lililojiri wiki iliyopita hotelini hapo, ilidaiwa kuwa
kisa cha yote hayo ni kufuatia Nora kudaiwa shilingi elfu tatu za
Kitanzania, deni aliloliacha kwenye gharama ya hoteli ambapo alitakiwa
kulipa shiling elfu 30.
Joyce alisema kuwa Nora
alifika hotelini hapo, akaomba chumba na alipoambiwa atoe fedha kwanza
aliomba udhamini aingie hotelini kisha atalipa mpenzi wake akifika.
Joyce
alidai kuwa walichukua muda wa nusu saa kukubaliana naye lakini baadaye
walimpigia meneja wa hoteli ambaye alikubali Nora apewe chumba.
Alidai
kuwa alipofika mpenzi wake ambaye ni mtu mzima, Nora alilipa shilingi
elfu 20 na kuacha deni la shilingi elfu 10 aliahidi kulipa wakati
anatoka.
Joyce alidai kuwa usiku Nora aliagiza chakula na wakati anakilipia
akampa mhudumu shilingi elfu saba badala ya shilingi elfu 10 ambapo
Joyce alizikataa. Baadaye meneja wa hoteli aliagiza zipokelewe.
Mhudumu
huyo alidai kuwa asubuhi wakati Nora anaondoka, alimzuia na kumdai ile
buku tatu na ndipo staa huyo akamzaba makofi huku akimkaba shingoni.
Joyce
alisema aliamua kwenda kumfungulia jalada la kesi katika Kituo cha
Polisi cha External, Dar kwa jalada namba RB/10153/2013-SHAMBULIO.
Joyce
alisema kuwa alishangaa alipofika polisi alikuta Nora ameshafungua kesi
akidai kufanyiwa fujo na kuibiwa fedha shilingi laki sita kwenye gari
lake ambapo kesi hiyo ilihamishiwa kituo kikubwa cha Mbezi Kwayusuf, Dar
lakini Nora hakutokea akiomba wayamalize mambo hayo.
Nora
alipopigiwa simu na alidai kuwa waandishi waandike
walichokisikia kutoka kwa Joyce kwani yeye hahitaji kuzungumza chochote.
No comments:
Post a Comment