MAMA SHARO AIKATAA DAMU YA SHARO MILIONEA
MAMA wa aliyekuwa msanii maarufu Bongo, marehemu Hussein Mkiety ‘Sharo
Millionea’, Zainab Mkiety amemkataa mtoto ambaye alipelekewa Tanga na
mama yake anayetokea Geita akidai ni damu ya Sharo.
Mtu wa karibu na familia hiyo amesema kuwa baada ya msiba
kupoa, mama wa mtoto huyo alifunga virago na mwanaye kwa ajili ya
kwenda kutembelea kaburi la Sharo na kwenda kujitambulisha kwa bibi wa
mtoto.
Chanzo hicho kilieleza kuwa mama mtoto huyo alipofika Muheza
jijini Tanga, alipokelewa na watu wa bodaboda ambao walimsindikiza hadi
nyumbani kwa mama Sharo.
“Alipofika alipokelewa lakini cha kushangaza
mama Sharo alimkataa na kusema marehemu hakuwa na mtoto kwa sababu
hakuwahi kumwambia,” alisema sosi huyo.
Ili kupata ukweli wa habari hiyo,tuliwasiliana na mama Sharo kwa simu ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Ni kweli alikuja mwanamke akiwa amebeba mtoto ambaye alijitambulisha kwangu kuwa ametokea Geita.
“Alisema
mtoto aliyekuwa amembeba ni wa Sharo lakini nilikataa nikamwambia kuwa
mwanangu hakuwahi kuniambia kuwa ana mtoto na nilipowauliza marafiki
zake walisema hawana taarifa hizo.
Nisingeweza kumpokea kwa sababu
alishajitokeza mwingine na kudai kuwa ana mimba ya mwanangu, baada ya
kumkataa mwanamke huyo aliondoka na mpaka leo sina mawasiliano naye.”
Sharo alifariki dunia kwa ajali ya gari Novemba 26, mwaka jana katika Kijiji cha Maguzoni-Soga, Wilaya ya Muheza jijini Tanga.
No comments:
Post a Comment