BABY MADAHA AONYWA KUHUSU UNGA NA POMBE
MWANADADA anayefanya vizuri katika anga la Muziki Bongo, Baby Joseph
Madaha, ametahadharishwa na baadhi ya wadau wa burudani hapa nchini
kutoshawishika na matumizi ya madawa ya kulevya pamoja na unywaji wa
pombe kupindukia kufuatia taarifa za hivi karibuni kuweka wazi mpango
wake wa kupiga kambi nchini Kenya.
Madaha ambaye ‘amekwaa dili’ la kufanya kazi chini ya Kampuni ya Candy
n’ Candy Records inayoongozwa na Joe Kairuki na iliyoko jijini
Nairobi, ameshauriwa hivyo kufuatia madai ya msanii mwenzake Rehema
Chalamila kutopea zaidi kwenye matumizi ya madawa hayo baada ya kuhamia
nchini humo kwa mgongo wa kazi ya muziki.
“Hatuna tatizo na Madaha
kwenda kufanya muziki Kenya, tunachotahadharisha ni kuwa makini ili
asije akaharibika kama Ray C ambaye alipokuwa Kenya ndiko alikozidisha
utumiaji unga na unywaji wa pombe kupitiliza, tunajua Madaha ni mfuasi
mzuri wa pombe, atulie na afanye kazi zake ,” alisema mdau mmoja wa
burudani aliyejitambulisha kwa jina moja la Marcus.
Baada ya kutafutwa Madaha kuzungumzia maoni hayo alisema: “Nakwenda
kufanya muziki wa kimataifa, nitapunguza starehe zisizo na ulazima na
kuhusu madawa ya kulevya hayana nafasi kwenye ubongo wangu
No comments:
Post a Comment