MWANAFUNZI
na mwalimu wake katika sanaa, Irene Uwoya na Lucy Komba wameingia katika bifu
zito chanzo kikidaiwa kuwa ni mwalimu huyo kumzunguka mwanafunzi wake kwa
mumewe, Hamad Ndikumana ‘Katauti’. Lucy ambaye ndiye mwalimu wa Uwoya kisanaa,
imedaiwa kuwa amemzunguka Uwoya kwa mumewe, Ndiku kwa kisingizio
cha kucheza naye filamu iliyofahamika kwa jina la Kwa nini Nisimuoe?
“Kimenuka! Lucy Komba amemhadaa
Ndiku, akazuga kuigiza naye filamu moja ndipo walipozama kwenye ukaribu
kwelikweli.
“Mbaya zaidi filamu yenyewe wameigiza
wahusika wawili tu (Lucy na Ndiku) mwanzo mwisho kule Tegeta. Sasa wewe
unafikiri kuna nini hapo kama siyo mapenzi?’’ kilihoji chanzo hicho makini.
Baada ya paparazi wetu kuyanasa madai
hayo, Jumatano iliyopita alimtafuta Uwoya kwa njia ya simu ambapo alipopewa
taarifa hizo, alionesha kushtuka na kuchanganyikiwa mumewe kuigiza filamu moja
na Lucy, alikata simu kisha baadaye akampigia paparazi yeye.
“Kuna wakati nilikuwa namtafuta Ndiku
sijui alipo kumbe alikuwa na Lucy, sawa lakini kama Lucy ameamua kunifundisha
mimi na sasa amemfundisha mume wangu sawa, tupo hapa!”
Paparazi wetu alihamishia majeshi kwa
kumtwangia ‘mtuhumiwa’, Lucy ambaye alitiririka kama ifuatavyo:
“Nilijua Uwoya akisikia itakuwa ni
balaa maana siku za nyuma niliwahi kumshutumu kutoka na mzazi mwenzangu
(Patrick Mbasha) lakini mimi nipo tayari kwa lolote!”
Lucy Komba ndiye aliyemuingiza Uwoya
kwenye sanaa baada ya kumchezesha Filamu ya Yolanda ambayo ndiyo
iliyomtambulisha vyema staa huyo kisha kuliteka soko la sinema Bongo.
No comments:
Post a Comment