KATIKA Dunia shida raha mitihani vyote ni kwa ajili ya mwanadamu lakini hayo yote ujenga maana tu pale mambo hayo yanapompata mwenzako, mwanadada Wastara Juma ‘Stara’ mwigizaji mahiri katika tasnia ya filamu Swahiliwood unaweza kumwita mwanamke shujaa katika maisha ya uhusiano, kwani toka mwanzo wa mahusiano yake na mwigizaji mwenzake marehemu Sajuki,maisha yao ni mitihani kila kukicha.
.
.
Stara anasema kuwa katika maisha yake kumejaa mikasa mateso na kila aina ya majaribu mengi sana hata anasema kuwa kwa mitihani aliyopitia anaamini kukomaa na kuwa kama mtu mzima kutokana na matukio yaliyomuandama toka siku ya kuanza maisha ya uchumba na Sajuki.
“Ni maisha yenye mitihani ya kila aina katika maisha yangu kabla ya ndoa yangu nilipata ajali ikiwa zimebaki siku chache tu kwa ajili ya ndoa yangu na mchumba wangu Sajuki, nilijuwa ilikuwa ndio mwisho wa maisha yangu na mwisho wa ndoa yangu, lakini Sajuki hakubadilika na alikuwa jirani nami,”anasema Stara.
.
.
No comments:
Post a Comment