msimu wa burudani Highlands fm 92.7

msimu wa burudani Highlands fm 92.7

Tuesday, May 28, 2013

BONGOMOVIE YAPATA SHAVU KWENYE ZIFF


ZIFF-Logo-on-WhiteBongomovie tushindwe sisi tu  time hii , baada ya kusemekana kwamba bongomovie ndiyo industry ya pili kwa ukubwa kwa uzalishaji wa filamu Africa baada ya Nigeria. Hiyo ni moja profile kubwa sana kwa tasnia kitu ambacho kitafanya macho ya wadau wa filamu Africa kuanza kuangalia hata na Tanzania.
Habari za uhakika kutoka kwa wadau wa ZIFF zinasema kwamba kwenye festival ya mwaka huu, ZIFF watatoa siku  moja  nzima kwa ajili ya kuonyesha filamu kutoka bongomovie tu ili kuwapa nafasi wazawa na pia kutambua juhudi zao kwa jinsi wanavyokuwa kwa kasi.ZIFF ni tamasha kubwa la filamu ambalo linajumuisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi. Nafasi nyingine ya bongomovie kuonekana na kufunguka nje ya mipaka ndiyo hii.

No comments:

Post a Comment