msimu wa burudani Highlands fm 92.7

msimu wa burudani Highlands fm 92.7

Tuesday, October 08, 2013

MAJUTO KUGOMBEA UBUNGE 2015


Habari tulizozipata zinasema kuwa gwiji la sanaa za vichekesho nchini, Amri Athumani 'King Majuto' ametangaza kugombea ubunge kwa 2015. Muigizaji huyu mkongwe mzee Majuto ametangaza  kugombea ubunge jimbo la Tanga mjini.
Majuto  mwenye umri  zaidi ya miaka 60 ametangaza nia yake hiyo alipohojiwa na Clouds, na akadai atagombea kupitia CCM. Bado tunamtafuta mzee majuto ili aweze kututhibitishia kama habari hizi ni kwa kweli au la na kama ni kweli ana mipango gani na jimbo hilo la Tanga mjini.

No comments:

Post a Comment