msimu wa burudani Highlands fm 92.7

msimu wa burudani Highlands fm 92.7

Thursday, October 03, 2013

PUMU YAMTESA JOKATE

MWANAMITINDO mwenye vipaji lukuki, Jokate Mwegelo amefunguka kuwa hali yake kiafya siyo nzuri, anasumbuliwa na ugonjwa wa pumu.

 Akipiga stori nyumbani kwao maeneo ya Kinondoni, jijini Dar, Jokate alisema kuwa anasumbuliwa na pumu ambayo huwa inamtokea mara kwa mara ambapo ikimtokea huwa inaambatana na homa kali ambayo inamfanya ashindwe kufanya kazi yoyote.
“Naumwa jamani, pumu inanisumbua inanitesa sana. Inaponitokea huwa nashindwa kufanya kabisa kazi zangu za kila siku na vitu vyote huwa vinalala hadi nitakapopata nafuu,” alisema Jokate kwa tabu.

No comments:

Post a Comment