msimu wa burudani Highlands fm 92.7

msimu wa burudani Highlands fm 92.7

Monday, September 30, 2013

WEMA KUFANYIA BETHIDEICHINA

 

JEURI ya Fedha! Wema Isaac Sepetu a.k.a Madam ameenda Hong Kong nchini China na kufanyia huko bonge la pati ya ‘bethidei’ yake wakati akitimiza umri wa miaka 25 huku staa mwenzake, Aunty Ezekiel akiungana naye akitokea Dubai.


Habari kutoka Hong Kong zilisema kuwa Madam alifanya tukio hilo Ijumaa iliyopita Septemba 27, mwaka huu ambapo aliongozana na ndugu yake aliyetajwa kwa jina moja la Bite huku Aunt akiungana naye akitokea kwa mumewe, Sunday Demont huko Dubai.
Taarifa kutoka huko zina dai kuwa aunt na wema walipiga vinywaji vikali

 Tukio hilo lilisababisha Wema kupokea hongera nyingi kutoka kwa mastaa wenzake, mashabiki na watu wa kawaida akisifiwa kuwa amewaziba midomo wasanii wenzake kwa kwenda kusherehekea siku yake ya kuzaliwa Hong Kong.
Akizungumza  kutoka Hong Kong, Aunt alisema kuwa alikwenda Dubai kwa mumewe lakini alikuwa na taarifa kuhusu pati ya Wema hivyo alivyofika Dubai alianza taratibu za safari za kuelekea Hong Kong.

No comments:

Post a Comment