msimu wa burudani Highlands fm 92.7

msimu wa burudani Highlands fm 92.7

Sunday, September 22, 2013

FILAMU 70 KUONYESHWA KTK TAMASHA LA AAFF 2013 JIJINI ARUSHA





KAMPUNI ya Hakika Entertainment inatarajia kuonesha filamu zaidi ya 70 kutoka nchi 20 katika tamasha la pili lijulikanalo kama Arusha African Film Festival (AAFF 2013), kuanzia Novemba 25 hadi Desemba Mosi, jijini Arusha.

 Kwa mujibu wa Mratibu wa AAFF, Nasir Mohamed, maandalizi ya tamasha hilo yameanza na filamu 70 kutoka nchi 20 za Afrika zitaoneshwa kwa siku saba. 

Nasir alisema, tamasha hilo litatanguliwa na semina, majadiliano, mafunzo sambamba na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali na kisha filamu hizo.

 “Tamasha la AAFF 2013, linatarajia kuwa la tofauti na kihistoria mwaka huu kwa wageni na watu watakaopata kuhudhuria tamasha hili kwenye viunga vya hoteli ya Mount Meru, Alliance Francois, hoteli ya New Arusha na Via Via,”
alisema Nasir.

 Kwa upande wake, Mkurugenzi wa AAFF, Akpor Otebele, alitoa rai kwa taasisi na kampuni kujitokeza kwa wingi kusapoti tamasha hilo ambalo limezidi kupata umaarufu. 

“AAFF ni tamasha ambalo linajenga umoja na ukaribu katika mawasiliano, biashara na mtandano wa kukuza sanaa hapa nchini,” alisema Otebele. 

 Tamasha hilo linatarajiwa kuhudhuriwa na zaidi ya watu 3,000 katika matukio makubwa huku wataalamu wa filamu, waongozaji, waigizaji, wasambazaji, wasanii na watu maarufu watahudhuria.

No comments:

Post a Comment