msimu wa burudani Highlands fm 92.7

msimu wa burudani Highlands fm 92.7

Thursday, August 29, 2013

MSANII WA FILAMU NUSURA APOTEZE MAISHA


MSANII wa filamu za Kibongo, Prisca Tadei hivi karibuni alinusurika kifo baada ya kupata ajali mbaya ya pikipiki wakati alipokuwa akielekea ‘location’ kushuti.
Ajali hiyo ilitokea wiki iliyopita maeneo ya Mbagala, jijini Dar ambapo Prisca aliumia vibaya sehemu mbalimbali za mwili wake baada ya pikipiki aliyokuwa amepanda kugongwa na gari ambapo alikimbizwa Hospitali ya Mnazi Mmoja na kulazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Akichonga , mkurugenzi wa kikundi anachofanyanacho kazi cha Kalunde Entertainment, Mariamu Athuman ‘Kalunde’ alisema anamshukuru Mungu kwa kuwa msanii wake huyo mpaka sasa anapumua na anaonesha matumaini kwani ilikuwa ajali mbaya.

No comments:

Post a Comment